Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025 | Msimu wa 2024-2025 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kwa jina la Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, unatarajiwa kuanza kwa kishindo Agosti 16, 2024. Msimu huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua zaidi huku timu 16 zikiwa zimechuana vikali kuwania ubingwa.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) imetangaza rasmi kuanza kwa msimu mpya wa 2024-25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 16, 2024.
Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025, Msimu huu unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na maboresho yaliyofanywa kwenye vikosi vya timu kadhaa ambazo zote zimeonyesha wazi nia ya kutaka kuipa changamoto Yanga Sc kutetea ubingwa wao.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, mashabiki wa soka watashuhudia mechi ya Ngao ya Jamii, itakayochezwa kati ya tarehe 8 na 11 Agosti 2024. Mechi hii ya jadi itakuwa kipimo cha awali cha uwezo wa timu kabla ya kuanza kwa msimu rasmi/Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025.
Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025
Msimu wa Ligi Kuu ya 2024/2025 utakuwa na raundi 30, ambapo kila timu itacheza dhidi ya nyingine mara mbili, nyumbani na ugenini. Msimu unatarajiwa kumalizika tarehe 24 Mei 2025, na kutakuwa na dirisha dogo la uhamisho lililofunguliwa kuanzia tarehe 15 Desemba 2024 hadi Januari 15, 2025, ambapo timu zitapata fursa ya kuimarisha vikosi vyao/Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025.
Ratiba Kamili ya Mechi za Wiki ya 26 NBC Premier League 2024/2025:
📅 Aprili 8, 2025
Pamba Jiji vs Fountain Gate FC – Saa 10:00 jioni (CCM Kirumba, Mwanza)
📅 Aprili 9, 2025
Kengold FC vs Tanzania Prisons – Saa 10:15 jioni (Sokoine Stadium, Mbeya)
Dodoma Jiji vs Kagera Sugar – Saa 1:00 usiku (Jamhuri Stadium, Dodoma)
📅 Aprili 10, 2025
JKT Tanzania vs Namungo FC – Saa 8:00 mchana (Mej. Jen. Isamuhyo, DSM)
Mashujaa FC vs Tabora United – Saa 10:00 jioni (Lake Tanganyika, Kigoma)
Coastal Union vs Singida BS – Saa 10:00 jioni (Mkwakwani Stadium, Tanga)
Azam FC vs Yanga SC – Saa 1:00 usiku (Azam Complex, DSM)
📅 Mei 11, 2025
KMC FC vs Simba SC – Saa 10:00 jioni (KMC Complex, DSM)

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa msimu wa 2023-2024 watakuwa na kibarua cha kutetea ubingwa wao dhidi ya timu nyingine kali. Msimu huu, Ligi Kuu itawakaribisha wapya Kengold FC kutoka Tukuyu, Mbeya, na Pamba Jiji FC ya Mwanza, ambazo zote zimepanda daraja kutoka Daraja la Kwanza/Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025.
Hii hapa Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025 kama ilivyo kwenye jedwali hapo chini:-
CHECK ALSO:
Weka maoni yako