Yanga Yatinga Fainali kwa Kuitoa Zimamoto Kwa Penati 3-1, Wakutana na JKU kwenye Kombe la Muungano 2025. Yanga SC, maarufu kwa jina la Wananchi, imetinga rasmi fainali ya Kombe la Visiwani Zanzibar baada ya kupata ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Zimamoto FC, kufuatia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC sasa itamenyana na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi) katika fainali ya michuano hiyo, baada ya JKU kuitoa Azam FC katika nusu fainali nyingine.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali, Zimamoto walionyesha ujasiri mkubwa na kupata bao la kusawazisha ndani ya dakika 90. Hata hivyo, mikwaju ya penalti ndiyo iliyoamua matokeo ya mechi hiyo, huku Yanga SC wakitumia uzoefu wao na ujasiri wa wachezaji wao kutinga fainali kwa ushindi wa mabao 3-1.
Yanga Yatinga Fainali kwa Kuitoa Zimamoto Kwa Penati 3-1

JKU yaiondoa Azam FC
Kwa upande mwingine, JKU waliendeleza ubabe kwa kuiondoa Azam FC, hatua iliyowapeleka fainali na hivyo kuweka rekodi nzuri kwa timu hiyo ya kijeshi ya Zanzibar.
Fainali inatarajiwa kuwa ya kusisimua:
Yanga SC dhidi ya JKU itakuwa fainali iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, ikizikutanisha timu mbili zilizopambana kutinga hatua ya fainali. The Citizens watakuwa wakihaha kutwaa taji hilo ikiwa ni sehemu ya harakati zao za kuelekea kwenye mechi muhimu za Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB.
CHECK ALSO:
- Wydad AC Yampa Mokwena Likizo Maalum, Mkataba Kusitishwa Mwisho wa Msimu
- Fountain Gate Yamtimua Kocha Matano, Amri na Khalid Kuchukua Mikoba Kumalizia Mechi 3
- Mtibwa Sugar Yapanda Ligi Kuu NBC Tanzania 2025/2026
- Raisi Samia Aahidi Milioni 30 Kila Bao Simba vs RS Berkane, Fainali CAF Confederation Cup 2025
Weka maoni yako