Ratiba ya Fainali Muungano Cup 2025, Yanga vs JKU – Tarehe, Saa na Uwanja. Kombe la Muungano 2025 imefikia kilele, na mechi ya fainali sasa itawakutanisha vigogo wa pande zote mbili za Muungano: Yanga SC kutoka Tanzania Bara dhidi ya JKU kutoka Zanzibar. Hii inatarajiwa kuwa mechi yenye ushindani na msisimko wa hali ya juu kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania na visiwani humo.
Ratiba ya Fainali Muungano Cup 2025, Yanga vs JKU
Mchezo: Fainali ya Muungano Cup 2025
Timu: Yanga SC 🟢 vs 🔵 JKU
Tarehe: 01 May 2025
Saa: 2:15 Usiku
Uwanja: Uwanja wa Gombani, Pemba Zanzibar
Yanga SC mabingwa wa Tanzania Bara wataingia fainali hii wakiwa na nia kubwa ya kuongeza taji lingine katika historia ya mafanikio yao. Kwa upande mwingine klabu ya JKU yenye historia ya mafanikio visiwani Zanzibar inatarajia kutumia nafasi hiyo ya kucheza nyumbani ili kuonesha ubora wao.

Mechi hii itakuwa ya kusisimua sana ikizingatiwa ni sehemu ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi.
Fainali ya Kombe la Muungano 2025 kati ya Yanga SC na JKU inatarajiwa kuwa ya kipekee na ya kusisimua. Hii si mechi ya soka pekee, bali pia ni ishara ya mshikamano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wapenzi wote wa michezo wanahimizwa kufuata matangazo rasmi kwa ratiba kamili na kujiandaa kwa burudani ya kipekee.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako